Sunday, January 22, 2017

Watu wasiofanya mazoezi ya mwili huzeeka haraka

Wanawake wenye umri mkubwa wanaoishi bila kufanya mazoezi, wanazeeka haraka kuliko wale hufanya mazoezi kila siku. Utafiti uliofanyiwa wanawake 1500 wenye umri wa kati ya miaka 64 na 95, uligundua kuwa wale waliotumia muda wao mwingi wakiwa wameketi na kufanya mazoezi yasiyozidi dakika 40 kwa siku, wana seli zenye umri miaka minane zaidi kibaolojia. Wakati watu wanazidi kuwa na umri mkubwa, seli zao nazo huzeeka. Watafiti kutoka Carlifonia wanasema kuwa watu wanastahili kufanya mazoezi hata wakati wa uzeeni na wazuie kuketi kwa zaidi ya masaa 10. Watafiti hao wanasema kuwa wakati mtu anapozeeka seli ndogo kwenye DNA huwa fupi kimaumbile.

0 comments:

Post a Comment