Sunday, January 22, 2017

Marekani: Nani watatumbuiza wakati wa kuapishwa kwa Donald Trump?

Wanamuziki wengi nyota walikataa kutumbuiza sherehe ya kuapishwa kwa Donald Trump. Wengi walikuwa wanamuunga mkono mpinzani wa Trump, Hillary Clinton, na hawakufurahishwa na sera za mwanachama huyo wa Republican hasa kuhusu wanawake, wahamiaji na dini. Lakini bado Bw Trump amewapata wanamuziki nyota wa kutumbuiza siku hii yake muhimu. Hata hivyo, wengine waandaa dansi mbadala za kumpinga. Mbona wanamuziki wamempuuza Trump? Kanye hatatumbuiza sherehe ya Trump Sherehe ya kuwakaribisha wageni Sherehe zilianza Alhamisi jioni kwa tamasha la Make America Great Again! (Rejeshea Marekani ukuu wake) katika sanamu ya ukumbusho wa Lincoln mjini Washington DC kama sehemu ya kuwakaribisha wageni. Waliotumbuiza ni pamoja na wanamuziki wa rock wa 3 Doors Down (pichani juu), ambao wamechomboa albamu mbili zilizokuwa nambari moja kwenye chati Marekani.

0 comments:

Post a Comment