Saturday, January 28, 2017

Arsene Wenger apigwa marufuku ya mechi nne

Mkufunzi wa Arsenal amepigwa marufuku ya mechi nne na faini ya paundi 25,000 baada ya kukiri mashtaka ya FA kwa tabia yake mbaya katika mechi dhidi ya Burnley. Wenger mwenye umri wa miaka 67 alishtakiwa kwa kumtusi na kumsukuma msaidizi wa refa Anthony Taylor baada ya kutakiwa kutoka uwanjani. Marufuku yake inaaza mara moja kwa hivyo atakosa mechi ya FA dhidi ya Southampton. Iwapo mechi hiyo italazimika kurudiwa ,Wenger atarudi uwanjani wakati wa mechi ya ligi ya Uingereza dhidi ya Hull mnamo tarehe 11 mwezi Februari. Hatahivyo iwapo mechi hiyo itakamilika siku ya Jumamosi na mshindi kubainika ,mechi dhidi ya Hull City itakuwa mechi yake ya nne na ya mwisho kuhudumia marufuku hiyo kufuatia mechi dhidi ya Watford na Chelsea.

0 comments:

Post a Comment