Trump ashambulia vyombo vya habari kufuatia picha za kuapishwa kwake

Siku moja baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kuchukua hatamu y a uongozi wa taifa hilo, amelaamu baadhi ya vyombo vya habari kwa kueneza taarifa za uongo juu ya idadi ya watu waliyohudhuria sherehe ya kuapishwa kwake.

Aliyekuwa rais wa Gambia Yahya Jammeh amewasili Equatorial Guinea

Aliyekuwa rais wa Gambia Yahya Jammeh amewasili nchini Equatorial Guinea, siku moja baada ya kuachia madaraka kwa Adama Barrow, aliyemshinda katika uchaguzi wa urais mwezi Disemba mwaka jana.

Arsenal yaishinda Burnley mabao 2-1

Alexis Sanchez aliifungia Arsenal bao la pili dakika ya 98 kwa njia ya Penalti na kuiweza kuwashinda Burnley mabao 2-1 nyumbani mwa Arsenal huko Emirates.

Diamond Platnumz – “Salome” ft. Rayvanny

This Song was written by Diamond Platnumz Rayvanny in Tanzania 2016 from Originally Song Maria Salome by Saida Karoli… The beat was produced, mixed and got Mastered by Lizer from Wasafi Records Tanzania….The Video was shot in Tanzania by Director Nicorux from South Africa, on the 10th of April 2016.

Maandamano ya wanawake dhidi ya Donald Trump, yamefanywa nchini Australia, New Zealand na Japani.

Maandamano makubwa kabisa hadi sasa yamefanywa Sydney, Australia, ambako watu kama elfu tatu wanaopinga ile inayosemekana kuwa tabia ya Bwana Trump, ya kunyanyasa wanawake, waliandamana hadi ubalozi mdogo wa Marekani mjini humo.

Sunday, May 14, 2017

Timu ya wasichana iliyoshinda ligi ya wavulana Hispania

Timu ya kandanda ya wasichana nchini uhispania imeibuka washindi katika ligi ya wanaume licha ya kutokuwepo uungwaji mkono kwa wanawake wacheza kandanda nchini humo. Timu hiyo ya AEM Lleida girls ishinda ligi ya pili ya wanaume kwa kushinda mechi 21 kat ya 22 ilizocheza. Mechi za kandanda zinazojumuisha jinsia zote uruhusiwa nchini Uhispania hadi wachezaji watimie miaka 14, na wasichana hawa wamecheza na wanaume tangu mwaka 2014. Hata hivyo hakuna ufadhili kwa timu yoyote ya wanawake hadi mwaka uliopita na hata klabu maarufu nchini humo ya Real Madrid haina timu ya wanawake. "Kuwawezesha wasichana hawa, tulihisi kuwa walistahili kucheza dhidi ya wavulana kwa sababu unahitaji wapinzani walio na uwezo ili kuweza kufanikiwa," mkurugenzi wa AEM Lleida Jose Maria Salmeron alisema.

Jambazi wa kike auawa na polisi Nairobi

Mwanamke anayedaiwa kuwa jambazi sugu, ambaye amekuwa akipakia mtandaoni picha zake akiwa amejipodoa na kujipamba, ameuawa na polisi jijini Nairobi. Kijana huyo ambaye ametambuliwa kama Claire Mwaniki aliuawa na polisi alfajiri na mapema Jumatano katika mtaa wa kayole. Gazeti la kibinafsi la Daily Nation linasema mwanamke huyo alikuwa na majambazi wengine wane wa kiume pale walipofumaniwa na polisi wakitekeleza wizi katika eneo la Lower Chokaa, mtaa wa Kayole. Anadaiwa kufyatulia risasi maafisa wa polisi akiwa na jambazi mwingine lakini wawili hao wakauawa. Wenzao walifanikiwa kutoroka.

Korea Kaskazini yalifanyia jaribio kombora la masafa marefu

Kumekuwa na shutma kubwa kote duniani dhidi ya hatua ya hivi punde ya Korea Kaskazini, kufanyia majaribio yake zana za nuklia Marekani inataka vikwazo zaidi viongezewe taifa hilo huku Ikulu ya White House ikisema kuwa, Pyongyang imechwa kutekeleza upumbavu kwa muda mrefu. Rais mpya wa Korea Kusini Moon Jae-in, amelaani kitendo hicho cha Korea Kaskazini, cha kufanya majaribio zaidi ya zana zake za mafasa marefu, akilitaja kama kitendo cha uchochezi. Jeshi la Marekani limetihibtisha kuwa kombora hilo la masafa marefu, lilirushwa karibu na mji wa kaskazini magharibi wa Kusong na kuanguka katika bahari ya Japan. Moon ambaye alisema anataka ushirikiano zaidi na utawala wa Pyongyang, wakati wa kampeni yake, amejibu hatua hiyo kwa kuitisha mkutano wa dharura na washauri wake wa kiusalama. Jaribio lingine la Korea Kaskazini la kuifanyia majaribio zana hizo, liligonga mwamba wiki mbili zilizopita.

Wednesday, April 12, 2017

Shambulio la Borussia Dortmund: Mshukiwa akamatwa

Maafisa wa polisi nchini UJerumani wanamzuilia mshukiwa mmoja anayehusishwa na itikadi kali za kiislamu kufuatia shambulio la bomu katika basi la timu ya Borussia Dortmund . Viongozi wa mashitaka pia wamesema kuwa vilipuzi vitatu vilikuwa vipande vya chuma. Maafisa wa polisi nchini Ujerumani wanachunguza uwezekano wa uhusiano wa kigaidi katika shambulio hilo , vyombo vya habari vya Ujerumani vimesema. Barua iliopatikana katika eneo la tukio inataja shambulio la krisimasi la mjini Berlin pamoja na operesheni za kijeshi nchini Syria. Haijabainika iwapo barua hiyo ilikuwa halisi. Wakati huohuo viongozi wa mashtaka nchini Ujerumani ambao huongoza uchunguzi unaohusishwa na ugaidi wanaongoza uchunguzi huo. Gazeti la Ujerumani la Sueddeutsch Zeitung lilisema kuwa barua hiyo inayoanza kwa ''Jina la mwenyezi mungu imesema Ujerumani inatumia ndege za Tornado katika muungano wa majeshi wanaopigana na Islamic State. IS imesema kuwa ilitekeleza mashambulio katika soko moja wakati wa Krisimasi mjini Berlin. Lakini kuna uwezekano washukiwa wanajaribu kuukanganya uchunguzi unaoendelea ,kulingana na gazeti hilo wakiongezea kwamba uchanganuzi wa barua hiyo unaofanywa na wataalam unaendelea. Shirika la habari la Ujerumani DPA pia limeripoti kwamba kuna barua ya pili inayosambazwa katika mitandao ya kijamii ikidai kuwa kundi la mafashisti lilitekeleza shambulio hilo. Barua ya pili ,ilichapisha maandishi ya kifashisti ikisema kuwa shambulio hilo linatokana hatua ya klabu hiyo kuwapendelea wafuasi wa mrengo wa kulia. Ni Nini kilichotokea? Borussia Dortmund ilikuwa ikielekea katika mechi ya vilabu bingwa ya robo fainali dhidi ya Monaco, wakati milipuko mitatu iliopotokea ,kulingana polisi. Picha kutoka eneo la tukio zinaonyesha madirisha ya basi hilo yakiwa yamevunjika huku matairi yakipasuka katika mlipuko huo. Mchezaji Marc Bartra alifanyiwa upasuaji baada ya kuvunjika mfupa katika kifundo chake cha mkono. Hakuna wachezaji wengine waliojeruhiwa lakini afisia mmoja wa polisi aliyekuwa katika pikipiki alisema kuwa ni shambulio lililopangwa. Ripoti kadhaa zilisema kuwa vilipuzi hivyo vilikuwa vimefichwa.

China na Marekani waitisha suluhisho la amani Korea kaskazini

Rais wa China Xi Jinping ameitisha suluhisho la amani kuhusu taharuki iliyotanda Korea kaskazini, katika maongeo ya simu baina ya rais wa Marekani na Donald Trump, vyombo vya habari China vimesema. Siku ya jumanne Trump aliandika kwenye mtandao wa kijamii tweeter kuwa Marekani haiogopi kupambana na Korea Kusini iwapo China haitasaidia. Hali ya taharuki ilitanda katika rasi ya Korea kusini baada ya kupelekwa kwa meli za kivita kutoka marekani katika eneo hilo. Korea kusini ilikasirishwa na hatua hii na ikajibu kwamba itajilinda vilivyo. Bwana Xi na Trump walikutana ana kwa ana wiki jana katika mkutano mjini Florida ambapo waliongea kuhusu Korea kusini. Mawasiliano yao ya simu yalifanywa jumatano asubuhi, kulingana na shirika la utangazi la China CCTV. White House bado haijatoa maelezo yoyote. Katika maongeo yao, Bwana Xi alisema kuwa China imejitolea kulinda amani na utulivu kwenye rasi ya Korea kusini na imeunga mkono kutafuta suluhisho kwa njia ya amani, CCTV ilisema.
Mapema jumatano, tahariri zilizochapishwa na shirika la utangazaji la Global Times ilitoa mwito kwa Korea kusini isizingatie amani mwanzo, ikinukuu kwamba Marekani haina mpango wa kuishi vyema na Pyongyang ambayo inamejihami na silaha za kinuklia. Trump alisema kuwa alimwelezea Rais wa China kwamba mkataba wa kibiashara na Marekani ina manufaa mazuri kwao iwapo watasuluhisha tatizo la Korea kusini. Katika mahojiano siku ya Jumanne katika shirika la utangazaji la Fox Business Network Marekani, Trump pia alisema "tunatuma armada ambayo ina nguvu zaidi. Pia tunazo nyambizi ambazo pia zina nguvu zaidi ya meli ya kubeba ndege."
Mapema wiki hii, kundi la Carl Vinson, ambayo inajumuisha meli ya kubeba ndege na meli nyingine ya kivita, zilibadilishwa njia kutoka Singapore hadi magharibi mwa bahari la Pacific ambapo ilifanya mazoezi na jeshi la mabaharia la Korea kusini. Jeshi la mabaharia la Japan pia limepanga mazoezi ya kijeshi na meli za kivita za marekani, shirika la habari la Reuters lilisema. Korea kusini imeongeza kufanya majaribio ya makombora miezi ya hivi karibuni, japokuwa imekatazwa na umoja wa mataifa dhidi ya matumizi ya nuklia na makombora

Mwanamke ambaka dereva wa teksi Marekani

Mwanamke mmoja katika jimbo la Ohio nchini Marekani ameshtakiwa kwa kum'baka dereva mmoja wa teksi kwa kutumia kisu kabla ya yeye na mwanamume mwengine kumuibia kulingana na maafisa wa polisi. Brittany Carter mwenye umri wa miaka 23, anadaiwa kufanya tendo la ngono na dereva huyo mwenye umri wa miaka 29 huku Corey Jackson mwenye umri wa miaka 20 akimshikia kisu shingoni. Maafisa wa polisi wanasema kuwa wawili hao waliiba dola 32 kutoka kwa mwathiriwa kabla ya kutoroka katika eneo la mkasa katika mji wa Findlay. Hatujui ni kwa nini alifanya hivyo,luteni wa polisi Robert Ting alisema.Pengine ilikuwa hali ya kumpumbaza kwa sababu pia walimuibia pesa . Unyanyasaji huo ulitokea baada ya bi Carter kumuita dereva wa teksi hiyo ya kampuni ya Trinity Express Cab mapema mnamo tarehe 28 mwezi Januari, kulingana na maafisa wa polisi. Alikamatwa baada ya dereva kuripoti kisa hicho . Bi Carter anakabiliwa na shtaka la ubakaji pamoja na lile la uhalifu katika mahakama ya kaunti ya Hancock. Alishtakiwa mara mbili kwa makosa ya dawa za kulevya mwaka 2016 na anadaiwa kumiliki dawa ya kulevya aina ya heroine. Bi Jackson hajakamatwa huku agizo la kukamtwa likitolewa kulingana na polisi. Anashtakiwa kwa kuchochea wizi na njama ya kutaka kufanya ubakaji.

Msichana anayeugua ugonjwa wa kuzeeka afariki A. Kusini

Afrika Kusini inaomboleza kifo cha Ontlametse Phalatse, msichana wa umri wa miaka 18 ambaye alikuwa anaishi na ugojwa unaojulikana kama Progeria, ambayo ni hali ya kimaumbile isiyo ya kawaida ambayo husababisha mtu kuzeeka kwa haraka. Mwezi uliopita Ontlametse alisherehekea siku ya kuzaliwa na rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma. Seriklia ya Afrika kuisni imeongoza taifa kutuma rambi rambi kufuatia kifo hicho. Alifariki hiyo jana katika hospitali ya Dr George Mukhari Academic iliyo nje ya mji wa Pretora.
Phalatse alikuwa mmoja wa wasichana wawili waliokuwa na hali hiyo nchini Afrika Kusini. Alijiita "mama wa kwanza" , baada ya kuwa mtoto wa kwanza mweusi nchini Afrika Kusini, kupatikana akiwa na ugonjwa wa Progeria. Alitajwa kuwa mtoto wa kuwapa watu motisha na mtot wa miujiza baada ya kuishi kuliko matarajio walioyokuwa nayo madaktari waliosema kuwa angefariki miaka minne iliyopita. Rais Zuma ametuma rambi rambi zake kwa familia ya msichana huyo.

Wanasayansi wanasa picha ya nyota zilizogongana

Wanasayansi wamerekodi picha za kusisimua zinazoonyesha nyota mbili changa zikigongana na kuharibu mpangilio wao. Nyota hizo ambazo ziko kwenye mkusanyiko wa Orion ziligongana miaka 500 iliyopita na kusababisha vumbi na gesi nyingi kuingia kwenye anga yao. Wanasayansi wanasema kugongana kwao kulitoa nguvu kiasi kama cha zile zinazoweza kutolewa na jua kwa muda wa miaka milioni kumi. Matukio yaliyojiri yamenakiliwa kwenye jarida la maumbile ya nyota. Nyota hutengezwa wakati wingu kubwa la gesi linapoanza kusambaratika. Kwa umbali wa miaka iliopita mwanga kutoka duniani, pamoja na nyota changa zilianza kuumbika katika wingu kubwa kwa jina Orion Molecular Cloud 1, (OMC - 1). Mvuto ulileta nyota hizo karibu kwa kasi sana hadi miaka 500 iliyopita, huku mbili kati yazo zikigongana ana kwa ana na kusababisha mlipuko mkubwa uliosambaza gesi na vumbi katika anga kwa kasi kubwa. Timu hiyo ya watafiti pia imegundua habari mpya kuhusu umbo la mwanga unaotokana na mlipuko huo. Wanasanyasi hao wanajifunza kuhusu mgawanyiko na mwendo wa gesi ya kaboni iliyo kule ndani. Hii itawawezesha kujua jinsi nyota inavyoumbwa.